Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tabaka mbalimbali za watu wa Yemen zimehakikisha zinatoa sapoti yao kamili kwa Iran na Gaza dhidi ya uhalifu wa Utawala haram wa Kizayuni unaofanya jinai zake kwa sapoti na msaada wa Marekani, ambapo wamejitokeza kwa wingi leo hii (Siku ya Ijumaa iliyoitwa: Ijumaa ya Ghadhabu na Ushindi) katika Maandamano makubwa katika maeneo kadhaa katika Mkoa wa Saada.
Katika Mkoa huo wa Saada Kaskazini mwa Yemen, kulishuhudiwa utaratibu wa maandamano 37 makubwa ya wananchi katika kituo cha Mkoa na Viunga vyake tofauti.
Maandamano haya yalifanyika kwa kauli mbiu hii: "Tumesimama na Gaza na Iran dhidi ya uhalifu wa Kiyahudi-Marekani", katika viwanja vya maeneo tofauti ya Mkoa wa Saada.
Washiriki wa maandamano haya waliidhinisha sapoti na msaada wao thabiti kwa Gaza na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ulinzi wa mambo mbalimbali matukufu ya Kiislamu.
Your Comment